Katika michezo 10 iliyopita kati ya Watford na Chelsea, Watford wameambulia suluhu mbili tu huku michezo nane iliyobaki wakichezea kipigo lakini Chelsea nao wameshindwa kupata hata pointi moja katika michezo yao miwili iliyopita ya Epl.
Manchester United nao hii leo watakuwa katika dimba la John Smith kukabiliana na Huddersfield huku wenyeji wakiwa na kumbukumbu ya miaka 46 iliyopita walipowakaribisha United na kuchezea kipigo cha bao 3.
United wanaingia katika mchezo huu wakiwa na rekodi nzuri sana msimu huu ambapo wakishinda wataweka rekodi ya kupata alama 23 ndani ya michezo 9 ya mwanzo ya ligi kuu huku wapinzani wao hawajashinda katika mechi 6 zilizopita.
Manchester City wakishinda katika mchezo wa leo wataweka rekodi mpya ndani ya klabu hiyo, rekodi ya kushinda michezo 11 mfululizo katika mashindano yote na watakuwa wameshinda michezo 7 mfululizo katika ligi kuu.
Katika mchezo mwingine Newcastle watacheza dhidi ya Crystal Palace, Swansea watawakaribisha Leicester City, Southampton dhidi ya West Bromich Albion na Fc Bournamouth watawafuata Stoke City.
No comments:
Post a Comment