![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjtRHf9OBfBGiAo6Beu4eCUP0fWXWrH6Vjbb4_WyWaXR_XcRRvVTLyiyibAh7m66nQ84ijlIBDYVNfqMs6ftWYK8XzXLKlbu9yvabVMuWo7BqJNh3DKRnPaftkE8yaB6fKj0KtR1YOqFcY5/s400/1.jpg)
Upande
wa utetezi wa kesi ya kutumia dawa za kulevya inayombili msanii, Agnes
Gerald maarufu kama Masogange utaanza kutoa ushahidi Novemba 14, 2017
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mshtakiwa
huyo alipaswa kuanza kujitetea leo Alhamisi lakini Wakili wa Serikali,
Adolf Mkini aliomba kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ipangiwe
tarehe nyingine.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 14, 2017.
Hatua
hiyo imefikiwa mara baada ya Hakimu Mashauri kumuona mshtakiwa huyo
kuwa ana kesi ya kujibu na kwamba anapaswa kujitetea na kuwaita
mashahidi wake.
Masogane anatetewa na mawakili Nehemia Nkoko na Ruben Simwanza.
Kesi
hiyo inaendeshwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula ambaye kwa
upande wao kuwaita mashahidi watatu wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi
wao na kuufunga.
Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha Sheria ya Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment