Prof.
Mwageni ameyasema hayo leo wakati anatoa ufafanuzi juu ya tarehe ya
kufunguliwa kwa vyuo kutokana na mkanganyiko ambao wameupata baadhi ya
wanafunzi kuhusu muda sahihi wa masomo kuanza kwa mwaka wa masomo
2017/18 hususani wale ambao wameomba nafasi kwenye awamu za pili na tatu
za Udahili.
“Tarehe ya Kalenda ya masomo
haijabadilika iko palepale ambayo ni Oktoba 30 wanafunzi wanatakiwa
kuanza masomo ya elimu ya juu kwa mwaka 2017/2018”, amesema Mwageni.
Aidha Prof. Mwageni ameeleza kuwa zaidi
ya wanafunzi 450,000 tayari wameshapata vyuo hivyo kinachosubiriwa
katika awamu ya tatu ni kupitisha wanafunzi wengine 12,000 ili kufikia
malengo ambayo ni wanafunzi 57,000.
Awamu ya tatu ambayo ilianza Oktoba 18
hadi 22 imefikia hatua nzuri ambapo vyuo vinawasilisha TCU majina ya
waombaji ambao vimewapitisha ili tume iweze kujiridhisha kisha wanafunzi
waliochaguliwa katika awamu hiyo wajiunge na vyuo na waanze masomo kwa
wakati.
Mapema mwaka huu Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alishauri TCU iweke utaratibu wa
wanafunzi kuomba nafasi chuoni moja kwa moja ili waende vyuo
wanavyotaka wao tofauti na awali ambapo zoezi la kupanga vyuo lilikuwa
linasimamiwa na Tume hiyo ya Vyuo Vikuu TCU
No comments:
Post a Comment