Friday, October 27, 2017

JULIO AWAPA SIMBA NENO JUU YA AJIBU

KOCHA wa Dodoma FC ya Dodoma, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameitaka timu yake ya zamani ya Simba kuwa makini na mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu leo kwani wakizubaa atawafunga.


Akizungumza na Championi Jumamosi, Julio alisema mchezo wa leo utakuwa mgumu na wenye
upinzani wa hali ya juu na Simba wasiwadharau Yanga hata kidogo.

Alisema Simba inatakiwa kumchunga Ajibu kwani wakizubaa kidogo tu atawafunga kwa jinsi kiwango chake kilivyo sasa.

“Ajibu ni mchezaji mzuri ana kiwango cha hali ya juu sio yule aliyekuwa Simba, hivyo ni mchezaji wa kuchungwa sana katika mchezo huu, akiachwa kidogo tu atawafunga,” alisema Julio.

No comments:

Post a Comment