Mcheza
tenisi huyo namba saba duniani alipata majeraha ya kiwiko cha mkono
mwanzoni mwa msimu huu na kushindwa kuendelea na michuano lakini sasa
yupo tayari kurejea kwenye michuano ya tenisi ya Abu Dhabi kuanzia
tarehe 28 hadi 30 Desemba.
"Nipo tayari kwa mapambano na wapinzani
wangu, nafikiri kitakuwa ni kipimo kizuri kwangu kurejea kwenye ubora”,
amesema Djokovic.
Naye mwanafainali wa michuano ya Wazi ya
Ufaransa Stan Wawrinka atakuwa anarejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa
muda mrefu akiuguza maumivu ya goti.
Wawrinka raia wa Uswis ambaye
anashikilia nafasi ya tisa duniani amekaa nje ya uwanja tangu mwezi
Agosti. Michuano ya Abu Dhabi itafanyika wiki mbili kabla ya kuanza kwa
michuano ya wazi ya Australia ambayo itakuwa michuano ya kwanza ya Grand
Slam ya msimu ujao.
Stan Wawrinka na Novak Djokovic
watachuana na wakali wengine akiwemo mchezaji namba moja duniani Rafael
Nadal, Dominic Thiem, Pablo Carreno Busta na Milos Raonic.
No comments:
Post a Comment