Alexandre
Lacazette akishangilia baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 74 katika
ushindi wa Arsenal wa 5-2 dhidi ya Everton leo Uwanja wa Goodison Park
kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England. Mabao mengine ya Arsenal
yamefungwa na Nacho Monreal dakika ya 40, Mesut Ozil dakika ya
53, Aaron Ramsey dakika ya 90 na Alexis Sanchez dakika ya 90 na ushei,
wakati ya Everton iliyomaliza pungufu baada ya mchezaji wake, Idrissa
Gueye kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya
njano yamefungwa na Wayne Rooney dakika ya 12 na Oumar Niasse dakika ya 90 na ushei
No comments:
Post a Comment