Sunday, October 22, 2017

Rais Robert Mugabe Awa Balozi







Shirika la Afya Duniani, WHO, limebatilisha uamuzi wake wa kumteua Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kuwa Balozi Mwema wa shirika hilo, kufuatia shutuma kali kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa WHO, Tedros Ghebreyesus, amesema amesikia malalamiko hayo na kuamua kubatilisha uteuzi huo.

Bw. Ghebreyesus ambaye awali aliisifu Zimbabwe kwa kujali afya ya wananchi wake, lakini wakosoaji wamedai kuwa, sekta ya afya nchini Zimbabwe imedhoofika chini ya utawala wa Rais Mugabe ambao sasa umedumu kwa miaka 30.

Wakosoaji wamedai watumishi wa afya nchini Zimbabwe mara nyingi hawalipwi mishahara, huku kukiwa na uhaba wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali na zahanati za umma.

Bw. Tedros, amesema, amewasiliana na serikali ya Zimbabwe kuhusu kubatilishwa kwa uteuzi wa Rais Mugabe kwa ajili ya manufaa ya shirika hilo la afya

No comments:

Post a Comment