![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSAIb_J0cGsKvWLvIWOD4miSr3nBzgycClMtHj6H3Cpo9C8fYLvnJgbUwtoU78M6mkqObu0RXIts7tzujZA96p5SQsw6FXLiiidw_Kex1bWtVAm3FzVsRZ-vCvtMsZcLtCw6JAAUQENq9R/s1600/1.jpg)
Kiongozi
wa madhehebu ya Ismailia duniani, Mtukufu Aga Khan ameondoka nchini leo
Alhamisi saa 7:25 mchana baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili
kwa mwaliko Rais John Magufuli.
Kiongozi
huyo ameagwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) na jumuiya ya
ismailia hapa nchini pamoja na viongozi wa Serikali ambao ni Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda.
Kikundi cha ngoma kilitoa burudani kwa kiongozi huyo kabla hajapanda ndege yake aina ya LX - PAK na kuanza safari.
Mtukufu
Aga Khan aliwasili nchini jana Jumatano saa 4 asubuhi akitokea Uganda
alikokwenda kuhudhuria sherehe za uhuru wa nchi hiyo kwa mwaliko wa Rais
Yoweri Museveni.
Akiwa
hapa nchini, Mtukufu Aga Khan alikutana na Rais Magufuli na kuzungumzia
mambo matatu ambayo ni afya, elimu na vyombo vya habari.
Katika
mazungumzo yao, Aga Khan aliahidi kushirikiana na Serikali katika kutoa
huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na mkakati wa taasisi zake kupanua
Hospitali ya Aga Khan na kujenga Chuo Kikuu cha Aga Khan huko Arusha
ambacho kitakuwa kikubwa.
Mtukufu
Aga Khan ndiyo mwasisi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) ambao
unatoa huduma mbalimbali nchini na sehemu nyingine duniani katika sekta
za afya, elimu, kilimo, fedha na bima.
No comments:
Post a Comment