Unaweza
kusema sasa ni uhakika kuwa Kocha Masoud Juma Irambona atakuwa katika
benchi la Simba Jumamosi.
Lakini itakuwa ni siku ya kwanza katika benchi
la moto kwa kuwa linaikutanisha Simba na mtani wake Yanga kwenye Uwanja
wa Uhuru.
Masoud
atakaa katika benchi la Simba kwa mara ya kwanza baada ya kuogopa
kufanya hivyo katika mechi iliyopita ambayo timu yake ilishinda 4-0.
Kocha
huyo alihofia kukaa kutokana na suaa la vibali vya kufanya kazi na
kulikuwa na taarifa Idara ya Uhamiaji walikuwa wanamsubiri kwa hamu.
Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa kila kitu kinashughulikiwa na leo au kesho.
"Mambo sasa ni uhakika, atakuwa katika benchi dhidi ya Yanga akisaidiaa na Kocha Omog," kilieleza chanzo.
No comments:
Post a Comment