Giggs
ambaye alikuwa msaidizi wa Louis Van Gaal ndani ya Manchester United
ameweka wazi nia yake hiyo wkaati akifanya mahoajiano na Sky Sports
kuhusiana na uelekeo wake kwenye kufundisha soka.
“Hizi ni klabu zinazonivutia
kuzifundisha kutoakana na aina yake ya uchezaji na zina wachezaji ambao
wana viwango bora”, amesma Giggs
Hata hivyo Giggs amegoma kuweka wazi
endapo atatuma maombi kwa uongozi wa timu hizo ili kumpatia nafasi hiyo
ya kuongoza benchi la ufundi.
Leicester City ilimfuta kazi kocha Craig
Shakespeare wiki iliyopita kabla ya jana Everton kumfuta kazi Ronald
Koeman. Giggs amekuwa nje ya masuala ya ukocha kwa kazi ya juu tangu
alipoondoka Manchester United mwaka 2016 baada ya mkuu wake Van Gaal
kuondolewa.
No comments:
Post a Comment