Tuesday, October 24, 2017

UN watoa tamko kuhusu wapinzani

Umoja wa mataifa umetoa wito ya kuachiwa mara moja kwa watu 30, wa chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutoka mahabusu
 
 
Wanachama wa vyama vikuu viwili vya Union for Democracy pamoja na wa Social Progress, walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, ulioko Kusini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya polisi kuvunja mkutano waliokuwa nao.
Imeripotiwa kwamba utawala wa Rais, Joseph Kabila, umepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa, pamoja na maandamano ya upinzani, tangu muda wake wa kukaa madarakani ka  kama Rais kisheria, ulipomalizika mwaka mmoja uliopita.
Hata hivyo imedaiwa kwamba maandamano ya mara kwa mara ya upinzani nchini humo umekabiliwa vikali na utawala wa Rais Joseph Kabila.
Kwa upande mwingine chama cha upinzani, Union for the Congolese Nation, kimesema kwamba, kitajiondoa katika serikali ya ugawanaji mamlaka, kutokana na kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu.
Tume ya uchaguzi nchini humo, imesema kuwa, haitakuwa rahisi kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais, kabla ya mwezi Aprili mwaka ujao wa 2019.

No comments:

Post a Comment