Mwanasheria wa Jumuiya ya Raia wa
Comoro waishio Tanzania, Larifou Said akizungumza na Waandishi wa habari
kuhusu tukio la kupotea kwa Mwanafunzi Raia wa nchi hiyo Ammar Abdousoi
Madou (pichani) ambapo waliliomba Jeshi la Polisi kusaidia upatikanaji
wa ndugu yao huyo.
JUMUIYA
ya raia wa Comoro waishio Tanzania wameiomba Serikali kupitia Jeshi la
Polisi nchini kusaidia kupatikana kwa ndugu yao Ammar Abdousoi Madou
(26) aliyepotea na kutoweka kusikojulikana tangu tarehe 29 Juni mwaka
huu.
Akizungumza
na Waandishi wa habari leo (jana) Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa
Jumuiya hiyo, Larifou Said alisema taarifa za kupotea kwa Madou ambaye
ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala nchini Uganda ziliifikia familia
yake tarehe 29 Juni, mwaka huu.
Said
anasema familia ya Madou ilipokea taarifa za kushikiliwa kwa Madou na
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha tarehe 27 Juni, mwaka huu kutoka kwa
rafiki wa karibu wa Madou anaeishi Mkoani Arusha na baadae kuelezwa kuwa
aliachiwa huru tarehe 29 Juni mwaka huu, ingawa tangu kipindi
hawajaweza kuonana nae hadi sasa.
Anasema
pamoja na familia hiyo kufanya jitihada mbalimbali za kufanikisha
upatikanaji wa ndugu yao ikiwemo kufanya Mawasiliano ya mara kwa mara na
vyombo vya usalama ikiwemo kuwasiliana na Idara ya upelelezi ya Jeshi
la Polisi kwa ajili ya kufahamu undani na sababu ya kukamatwa kwa Madou.
Akifafanua
zaidi Said anasema Jumuiya hiyo tayari imefanya mawasiliano na Ubalozi
wa Komoro nchini, ambao nao uliandika barua katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuelezea malalamiko yao ya
kupotea kwa ndugu yao ambapo pamoja na kuomba uchunguzi wa kina uendelee
kufanywa na vyombo vya dola vya Tanzania.
“Wiki
iliyopita tulielezwa na Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Arusha kuwa Madou aliachiwa huru, lakini tulipofunga safari kuelekea
Arusha hatukumkuta bado tunaendelea kujenga imani na vyombo vya dola vya
Tanzania lakini tunaomba jitihada ziendelee kuongezwa ili Madou aweze
kupatikana” alisema Madou.
Akielezea
tukio la kukamatwa kwa Madou alisema, ndugu yao alirudi Tanzania mwezi
juni mwaka huu kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Idd el fitri ambapo
tarehe 27 juni mwaka akiwa njiani kurudi Uganda alikamatwa Moshi Mkoani
Kilimanjaro akiwa katika basi yenye namba za Usajili T 502 DHF na baadae
kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Arusha.
Said
anasema pamoja sheria kulitaka Jeshi hilo kumfikisha mtuhuhiwa
mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili, Ofisi ya Polisi
ilishindwa kumfikisha mtuhumiwa huyo katika mhimili wa dola na baadae
kudai kuwa lilimwachia huru pasipo na kupatikana kwa vielelezo
vinavyoonyeshwa kuachiwa kwake.
No comments:
Post a Comment