Friday, October 20, 2017

Mesut Ozil hali imekuwa sintofahamu Arsenal










Mesut Ozil bado hali yake katika klabu ya Arsenal imekuwa ya sintofahamu, kiungo huyo Mjerumani hadi sasa hajasaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo huku ule alio nao unakaribia kuisha.

Mesut Ozil anataka kulipwa mshahara wa £350,000 kwa wiki kiasi ambacho Arsenal wamesema hawana na kutaka kumpa £280,000 pesa ambayo Mesut Ozil na wawakilishi wake wameikataa.
Kwa hali ilivyo ni wazi kwamba dirisha lijalo la usajili Mesut Ozil pamoja na Alexis Sanchez wanaweza kuondoka bure katika klabu hiyo kwani wote wawili mikataba yao inafikia ukingoni.
Manchester United wanaguatilia mienendo ya suala la Ozil na Sanchez kwa ukaribu lakini sasa inasemekana Manchester United wako katika nafasi nzuri kumchukua Mesut Ozil dirisha la January.
Mesut Ozil ana uhusiano mzuri sana na kocha wa United Jose Mourinho na walishawahi kufanya kazi pamoja jambo ambalo linaonekana linaweza kumvuta Mesut Ozil akakipige Old Traford.
Mesut ameshawaambia marafiki zake kuhusu kuungana tena na Jose Mourinho huku kocha Arsene Wenger naye akithibitisha kwamba Ozil na Sanchez wote wanaweza kuondoka katika dirisha lijalo la usajili.
Wenger amesema suala la Sanchez na Ozil wamejaribu kila kitu na kuna uwezekano wa lolote kutokea japo wachezaji hao wote wawili wanaonekana wana furaha katika kikosi cha Arsenal

No comments:

Post a Comment