Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton huenda leo akaibuka bingwa wa mbio za magari duniani Formula1 endapo atashinda kwa pointi nyingi kwenye mbio za leo nchini Marekani (USGP).
Hata hivyo Hamilton ana nafasi ya
kufanya hivyo baada ya kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye mpangilio
wa magari wakati wa mbio hizo. Mkali huyo wa gia kutoka nchini Uingereza
ameongoza mbio za kusaka nafasi kwenye kupanga magari ambapo sasa leo
ataanza wa kwanza.
Mpinzani wake wa karibu Sebastian Vettel
kutoka timu ya Ferrari amemaliza wa pili hivyo gari yake itasimama
kwenye nafasi ya pili wakati wa mbio za USGP leo akifuatiwa na gari ya
Valtteri Bottas wa Mercedes ambaye atakuwa wa tatu.
Mbio zitafanyika jioni ya leo kwenye
mitaa ya Austin jijini Texas Marekani. Hadi sasa Lewis Hamilton
anaongoza mbio hizo akiwa na alama 306 mbele ya Sebastian Vettel mwenye
pointi 247.
Baada ya mbio za leo za USGP zitakuwa zimebaki mbio 3 ili kumaliza
msimu wa 2017 ambazo ni Mexico Grand Prix, Brazilian Grand Prix na Abu
Dhabi Grand Prix.
No comments:
Post a Comment