Saturday, October 7, 2017

AFRIKA KUSINI YAILAZA 3-0 BUKINA FASO

Sibusizo Vilakazi wa Afrika Kusini akisherehekea bao lake dhidi ya Burkina Fasso

Afrika Kusini ilijipatia matokeo mazuri katika kampeni yake ya kutaka kufuzu katika kombe la dunia baada ya kuifunga Burkina Faso 3-1 mjini Johannesburg.

Percy Tasu aliwapatia wenyeji uongozi wa mapema , Themba Zwane akaongeza idadi hiyo na kuwa mabao mawili baada ya nusu saa kabla ya Sibusizo Vilakazi kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ya kipindi cha kupumzika.
Bongani Zungu alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 69 kwa ukosefu wa nidhamu kufuatia mgogoro.
Mchezaji wa Burkina Faso Alain Traore alikuwa na bahati kusalia uwanjani baada ya kumpiga kisukusuku Zungu.

No comments:

Post a Comment