Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya
ambaye ndoa yake na mchezaji mpira Ndikumana Katauti wa Rwanda iliingia
katika mgogoro mzito na kupelekea kila mtu kuishi peke yake amefunguka
na kuwataka watu wasimuingilie katika malezi ya mtoto wake.
Msanii Irene Uwoya.
"Wale mnaosema namlea kizembe naombeni sana mniache, namlea navyoweza mimi na mwanangu bado mdogo sana anahitaji mapenzi ya Mama. Hakuna hata mmoja wenu amewahi kuchangia ata mia ...sipendi kuongea sababu siyo swaga zangu, mimi mpole sana ila kwa mwanangu sina masihara. Sijawahi sema kitu ila leo nimeona niseme na sitarudia tena kusema, mwenye maskio na asikie na mwenye macho aoneee! yale mambo ya laaana mnayo mtabiria mwanangu yashindwe na MUNGU awasamehe sababu hamjui mlitendalo" alisisitiza Irene Uwoya.
No comments:
Post a Comment