Sunday, October 22, 2017

Manchester United wakubali kichapo,Mourinho amchana Ander Herrera


Kwa mara ya kwanza hapo jana Manchester United walikubali kuchezea kichapo katika msimu huu, United wakiwa ugenini walikubali kipigo cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa timu iliyopanda daraja ya Huddersfield.

Baada ya mchezo kuisha kiungo wa Manchester United Ander Herrera alidai kwamba wapinzani wao walijituma zaidi haswa katika dakika 30 za mwanzo kuliko vile ambavyo Manchester United walijituma.
Baada ya kauli hiyo ya Herrera kocha wa Manchester United Jose Mourinho naye alisema yake na kuonesha wazi kwamba hajapendezwa na majibu ya Herrera kuhusu dakika 30 za mwanzo za mchezo huo.
Mourinho anasema inasikitisha sana kwa mchezaji kama Hererra kusema kwamba walizidiwa katika kujituma na ni mbaya sana, Mourinho anasema bora kwake kama kocha lakini kauli ya namna hiyo haiwafanyi mashabiki kujisikia vizuri.
Lakini Mourinho amekiri kwamba Hudders walikuwa vizuri sana na wameshinda kwa kuwa walikuwa vizuri zaidi yao huku akishangazwa na namna walivyokuwa akikiri kwamba hakutegemea wangekuja hivyo.
Kipigo cha Manchester United kimeongeza pengo la alama kati yao na Manchester City ambapo kwa sasa Manchester City wanaongoza ligi wakiwa na tofauti ya alama 5 na anayewafuatia.

No comments:

Post a Comment