![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgEWq8Hc9gXBnuAM5uClSMCJV6nPFFWyDFrugYXCAysaivloKFtnQWnU2e3qoAMWNEwFbLF2b6bEHx0dt-K0R7JZYhwBlDOSfy2JZ34wxW814nC5ijBuddow0-NsVk-riecmnE0qAB_x4rA/s1600/1.jpg)
WATU
watano wakazi wa Wilaya ya Igunga wamefariki duniani katika matukio
mawili tofauti kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tabora.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa amesema hayo leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Alisema
kuwa katika tukio la kwanza mnamo tarehe 11 mwezi huu, watu wanne
wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba waliyokuwa
wakiishi kufuatia mvua zilizonyesha kwa kipindi cha siku mbili.
Kamanda
Mtafungwa alisema waliofariki kwa kuangukiwa na ukuta wanatoka kijiji
cha Igogo kata ya Nanga na aliwataja kwa majini kuwa ni Kagwa
Makenza(80) ambaye pia ni mmiliki wa nyumba iliyosababisha maafa hayo,
wengine ni Sande Dule (6), Butonda Shija(3) na Mbula Dule mwenye miezi
miwili.
Alisema watoto wote watatu walifariki dunia wakati wakipata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.
Katika
tukio la Pili , Kamanda Mtafungwa alisema katika kijiji cha
Bulyang’ombe kata ya Nanga mtoto Zenga Tano (5) alifariki dunia baada ya
kupigwa na radi mnamo tarehe 10 mwezi huu wakati amelala na wazazi
wake.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alitoa pole kwa familia za
waliopatwa maafa na kuwashauri wakazi wa Igunga kufuata utalaamu wa
ujenzi wakati wa ujenzi wa nyumba zao ili kuepuka maafa zaidi.
Alisema kuwa ushauri huo ni pamoja na ujenzi katika sehemu ya miinuko kwa ajili ya kujikinga na maafa zaidi.
No comments:
Post a Comment