Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho amekanusha taarifa za kuwa maneno yake aliyosema kuhusu makocha
wanaolia yalikuwa yanamlenga kocha wa Chelsea Antonio Conte.
Meneja
huyo raia wa Ureno amesisitiza kuwa hakumlenga Antonio Conte aliposema
kuwa hafurahishwi na makocha wanaolia kuwa na majeruhi kwenye timu zao.
Wawili hao wamekuwa na majibizano siku
za hivi karibuni lakini Mourinho amesema hana ugomvi na kocha huyo labda
kama yeye anashida binafsi na Mreno huyo.
"Sizungumzi naye, sijui kwa nini
anaongea na mimi lakini sio shida au labda si kosa lake ni kosa la
waandishi wa habari wanapompa ujumbe usio sahihi," amesema Mourinho.
No comments:
Post a Comment